Rushwa ndogo ndogo katika huduma za afya - 2010
HII ni ripoti ya utafiti uliafanyika kwa agizo la Sikika, shirika linalofanya
shughuli za maendeleo ya jamii hususan katika sekta ya afya.
Rushwa ni tatizo linagusa sekta zote, lakini ni tatizo kubwa zaidi
katika sekta ya afya. Hii ni kwa sababu inapunguza rasilimali
muhimu zinazotengwa kwa ajili ya afya, inapunguza ubora na
ufanisi katika utoaji wa huduma za afya na kuongeza gharama za
huduma, vilevile rushwa inaondoa usawa katika upatikanaji wa
huduma za afya kwa kuwakatisha tamaa watu ambao hulazimika
kufanya malipo ndipo wapate huduma. Hatimaye rushwa
inasababisha kushuka kwa viwango vya huduma za afya kwa
umma.
Ripoti ya Warioba (JMT, 1996) ilibainisha kwamba rushwa ni
tatizo kubwa katika sekta ya afya. Hata hivyo, kwa mujibu wa hadidu
za rejea za utafiti huu (YAV, 2007), kuna uhaba wa takwimu
zinazozungumzia rushwa katika mfumo wa utoaji wa huduma za
afya; hususani katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani; maeneo
ambayo Sikika inaendesha shughuli zake. Taarifa zilizofanyiwa
utafiti zinahitajika ili kutoa mwanga juu ya masuala yanayohusiana
na kuimarisha njia za kuzuia na kupambana na rushwa katika
mfumo ya utoaji huduma ya afya.
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza hali ya rushwa katika
utoaji huduma za afya kwenye wilaya nne za Kinondoni, Temeke,
Ilala na Kibaha na kupendekeza namna ya kuitokomeza.
Download file
Comments
|