LANGUAGE :
English | Swahili

Publication categories

Chakula Cha Daktari - Juni 2010

Kama ilivyo katika nchi nyingine, nchini Tanzania pia, rushwa imeenea katika sekta
zote za uchumi na utumishi wa umma kiasi kwamba imekuwa ni sehemu ya maisha
ya kila siku ya mtanzania. Ripoti ya Warioba (URT, 1996) imewasilisha ushahidi
kwamba hata maafisa katika vyombo vya serikali vilivyokabidhiwa dhamana ya
utawala wa sheria kama Usalama wa Taifa, Polisi, Mahakama, na Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa vinajihusisha na rushwa. Kwa miaka mingi, wanaotoa na
kupokea rushwa wanaonekana kuikubali na kuona ni kitendo cha kawaida. Matokeo
yake, sehemu kubwa ya jamii inaamini kwamba bila kuhonga hawatahudumiwa
ipasavyo. Kuenea kwa rushwa kunadhihirishwa na kupanuka kwa msamiati: rushwa,
hongo na mulungula ni baadhi tu ya maneno yanayotumika kwa muda mrefu. Lakini
wale wanaoshawishi kupewa rushwa kwa kawaida hutumia maneno 'laini' na
matamu kama vile; kitu kidogo, chai na mshiko ili kuhalalisha vitendo vyao.


Rushwa ni tatizo kubwa linalogusa sekta zote, lakini ni tatizo kubwa zaidi katika sekta
ya afya kwa sababu inapunguza rasilimali muhimu zilizo tengwa kwa ajili ya kutolea
huduma za afya. Pia, hupunguza ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma za afya na
huongeza gharama za huduma za huduma hizo. Vilevile, rushwa inapunguza usawa
katika upatikanaji wa huduma za afya kwa kuwakatisha tamaa masikini, ambao
wanalazimika kutoa rushwa ili kupata huduma zinazostahili kutolewa bure. Matokeo
yake ni kushuka kwa kiwango cha afya na ustawi wa jamii. Muhtasari huu
unawasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na Sikika mwaka 2007 kuhusu 'Rushwa
katika Utoaji wa Huduma za Afya katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani

Download file

 

Comments

    To leave a comment please fill the following form