Karibu Sikika

Sikika ni shirika lisilo la kiserika lililosajiliwa nchini Tanzania kwa lengo la kufanya ushawishi na utetezi juu ya utawala bora katika sekta ya afya. Shirika lilianzishwa mwaka 1999 likijulikana kama Youth Action Volunteers (YAV). Baadaye lilikua na kubadilika kutoka katika utetezi wa afya ya uzazi kwa vijana na kujikita kwenye kutetea mambo yafuatayo katika sekta ya afya: Ongezeko la bajeti, uwazi na uwajibikaji, Kukabiliana na upungufu wa rasilimali watu, Uwepo na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuhimiza Uwajibikaji katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali za UKIMWI.

Tumeendelea kufanya tafiti mbalimbali za kitaalamu na kutumia matokeo ya tafiti hizo kufanya utetezi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya. Shirika, kwa kutambua mchango wa watoa huduma na wananchi ambao ni watumia huduma, linaendelea kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kuchambua na kutathmini taarifa zinazohusu utoaji na upatikanaji wa huduma za afya katika ngazi zote kupitia mafunzo ya Usimamizi wa Uwajibikaji wa Jamii (SAM) na kufuatilia utekelezaji wake.

Sikiliza vipindi vyetu vya radio

 

SAM: Inachangia vipi kuboresha huduma za afya?

SHUGHULI ZETU

HEALTH-CARE-GOVERNANCE-AND-FINANCING-HGF

Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya

Idara ya Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya inafanya…

MEDICINES-AND-MEDICAL-SUPPLIES-MS- (1)

Dawa na Vifaa tiba

Idara hii ina lengo kuu la kuboresha uwepo na upatikanaji…

HIV-AIDS

VVU/UKIMWI

Idara ya VVU/UKIMWI inalenga kuhimiza uwajibikaji katika usimamizi wa matumizi…

HUMAN-RESOURCE-FOR-HEALTH-HRH

Rasilimali Watu

Idara hii inalenga kuona ongezeko la bajeti ili kukabiliana na…

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors