


Juu yetuShuguli za SikikaKwa sasa sikika inatekeleza mpango na mkakati wake wa mwaka 2010-2011, mpango ambao upo katika makundi matatu kama itavyoelezwa badae katika ukurasa huu. Dhumuni kuu la mpango huu ni kuhakikisha ubora na usawa katika mifumo ya utoaji wa huduma za afya pamoja na uwajibikaji katika ngazi zote za serikali. Ili kufikia lengo hili shughuli za sikika zinalenga maeneo makuu matatu nayo ni: Usimamizi wa huduma za afya na fedhaDhumuni: kuboresha bajeti na ufanisi katika secta ya afya vvu na ukimwi, uwazi na uwajibikaji katika serikali kuu pamoja na serikali za mitaa. Kipengele hiki kinaelenga kuhamasisha watungaji sera ili kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika kupanga bajeti, hii itajumuisha kufanya tathmini ya kina ya bajeti ya afya katika seta ya vvu na ukimwi ili kutambua kama mgawanyo wa fedha umegawanya kadiri ya mipango, sera na vipaumbele husika. Pia tutatathmini jinsi makundi tofauti wakiwemo wabunge pamoja na wananchi wanapata taarifa za bajeti.
Ili kuboresha usimamizi wa maliasili ya uma, sikika inahusika na kufanya tathmini ya namna gani mamlaka husika katika ngazi ya wilaya na taifa wanafanya nini ili kuziboresha huduma za afya, tunatumia redio pamoja, machapisho pamoja na njia nyingine za habari kukuza uelewa pamoja na kuibua majadiliano baina ya wanajamii juu ya matumizi mabaya ya rasilimali katika secta afya na janga la ukimwi. Tunahimiza wananchi kudai taarifa kutoka kwa vinongozi wao pamoja na watoa huduma na kushirika kikamilifu katika kudai matumizi mazuri ya rasilimali.
Rasilimali watu katika afyaDhumuni: kuboresha uwajibikaji na mgwanyo sawa wa wafanayakazi wa afya katika sehemu zote za utoaji wa huduma. Lengo la msingi la kipengele hiki ni kuboresha ufanisi, usawa na bajeti ya wafanyakazi wa afya. Katika kutimiza hili sikika hufanya tathmini ya bajeti ya secta ya afya, mipango, pamoja na taarifa za matumizi kuhusiana na mafunzo, kuajiri na usawa wa nafasi, tunakusanya taarifa kutoka ngazi za chini kuhusiana na ukubwa wa kazi pamoja na muda wanaosubiri katika vituo vya afya ili kupata taarifa juu ya usawa wa mgawanyo wa wafanyakazi wa afya kitika wilaya kulingana na bajeti iliopangwa. ili Kuboresha usawa wa mafunzo, mgawanyo, na kubaki kwa wafanyakazi wa afya katika ngazi zote huwa tunafanya tafiti ya mgawanyo na kubaki kwa wafanya kazi ili kupata taarifa pamoja na kupigania usawa kati ya wafanyakazi wote katika nyaja zote. Ili kukuza uelewa wa wafanyakazi juu ya maadili ya kazi, sikika hufanaya tafiti na kukusanya taarifa kuto kwa wananchi, rushwa, lugha chafu, pamoja na kuzingatia maadili ya kazi ni vitu ambavyo hufanyiwa tafiti. Madawa na ugawajiDhumuni: kuongeza uwazi na uwajibikaji katika manunuzi na usambazaji wa madawa bora, vifaa vya afya katika ngazi zote za utoaji wa huduma Kipengele hiki hulenga ufanisi katika manunuzi, uzambazaji, na uhifadhi wa madawa ni bora. Ili kuboresha ufanisi pamoja na usawa katika mipango pamoja na kupanga bajeti kwa ajili ya madawa bora, sikika hukusanya taarifa juu ya kiasi gani cha madawa kimeagizwa kusambazwa katiaka vituo vya afya na kiasi gani cha madawa kimepokelewa na vituo husika ikilinganishwa na bajeti iliyopangwa. Sikika pia inahamasisha wananchi kukusanya taarifa za usambazaji wa madawa katika bohari za uzambazaji. Ili kuboresha ufanisi na uwazi katika manunuzi na uzambazaji wa madawa sikika hufuatilia ni madawa gani yapo katika bohari na ni madwa gani huzambazwa katika vituo vya afya. |