


Juu YetuHistoria yetuSikika ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa mwaka 1999 kama youth action volunteers (YAV). Lengo kuu la shirika wakati huo lilikuwa ni kuwawezesha vijana kama gurudumu la kuleta maendeleo ili kuwa na taifa bora na linalowajibika. Shirika lilijisajili upaya mwaka 2009 sio tu kwa kubadili jina na kuwa “sikika” bali pamoja na kubadili mtazamo wake na kujumuisha wananchi wote. Tangu hapo shirika limekuwa likijitahidi kuhakikisha wananchi wanahimizwa kushiriki katika mipango ya maendeleo ya taifa ili kutambua mpango wa maendeleo ya taifa kwa mwaka 2025
Kwa miaka mitano sasa, sikika imejikita katika maeneo makuu ya kazi nayo ni mabadiliko yakinifu katika masuala ya afya pamoja na sera na mazingira ya bajeti katika masuala ya vvu na ukimwi.uzoefu wa sikika kwa sasa unawekwa katika utekelezaji katika mipango na mikakati yake ya mwaka (2011-2015) ambapo ushiriki mzuri wa wananchi katika utungaji wa sera, mapitio ya bajeti pamoja na upangaji wa bajeti katika sekta ya afya hususan vvu na ukimwi huwa na nafasi kubwa.
Wapi tunafanya kaziKwa saa sikika tunafanya kazi katika jiji la Dar es salaam katika wilaya za kinondoni, Temeke, Ilala pamoja na Kibaha katika mkoa wa pwani. Kutokana na sensa ya Tanzania ya mwaka 2002 jiji la Dar es salaam lina watu 2,497,940 na mji wa Kibaha una watu 132,045.
Sikika tunafanyaje kaziPamoja na wafanyakazi wake, sikika hushirikisha wafanyakazi wa kujitolea ambao hufikia jumuia mbalimbali katika jamii, kwa sasa sikika hufanya kazi na wafanyakazi wa kujtolea 70 kutoka mkoa wa Dar es salaam na wilaya ya Kibaha. Shirika pia hufanya kazi kwa kushirikiana na mashirika mengine yasio ya kiserikali na mitandao mingine katika kutimiza malengo yake, kwa kupitia uhshirikiano huu sikika inaweza kutekeleza sera na kazi zake. |