Fafanuzi

  
Maoni yetu juu ya repoti ya ukaguzi wa fedha wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa mwaka 1998/99-2006/07

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilianzishwa chini ya Ibara ya 143, ibara ndogo ya 5 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu za serikali na asasi nyingine za umma. Sheria ya Fedha namba 6 ya mwaka 2001 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004 inampa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu mamlaka ya kukagua hesabu za asasi za umma angalau mara moja kila mwaka.
Uchambuzi huu unapitia kwa kina ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi yamechukuliwa kama taarifa sahihi katika kupima uwajibikaji kifedha wizarani.
Toleo jipya la ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi inapendekeza uboreshaji wa jumla wa usimamizi wa fedha serikalini (soma Jedwali 1). Kuanzia mwaka wa fedha 2005/2006 hadi 2006/2007, hati safi zimeongezeka kutoka asilimia 57 hadi asilimia 77, wakati hati chafu zimepungua kutoka asilimia 39 hadi 26 na hati zenye hitilafu zimepungua kutoka asilimia 4 hadi sifuri.

Soma zaidi


Maoni kuhusu Afya ya Mama na Mtoto – 2006/2007

Muhtasari huu unatokana na ushirikiano kati ya YAV, Asasi ya Usawa katika Afya na Kamati za Bunge za Huduma za Jamii na Ustawi wa Jamii wenye lengo la kuchangia katika jitihada kupunguza vifo vya wanawake wajawazito. Mpaka sasa jitihada za wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika mapambano haya hazijafanikiwa na wala hazikaribii mafanikio. YAV imepitia maswali na majibu yaliyoulizwa bungeni wakati wa kikao cha bunge na inawasilisha yaliyojitokeza katika muhtasari huu wa sera.

Soma zaidi


Maoni kuhusu bajeti ya sekta ya afya – 2007/2008

Ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma (PER) ni moja kati ya vipengele vya mchakato wa mipango na bajeti ya serikali, vyenye lengo la kuhakikisha mfumo wa matumizi ya serikali unarandana na vipaumbele vya kisera kama vilivyo ainishwa katika mkakati wa kupunguza umasikini, ambao ni mkakati wa muda wa kati wa kupunguza umasikini ulioanzishwa kwa ushirikiano kati ya wadau wa kitaifa na wa kimataifa. Aidha, ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma ni kipengele muhimu katika Ukaguzi wa Mwaka wa Sekta ya Afya (AJHSR). Kwa kawaida hufanyika katik robo ya pili ya mwaka wa fedha kama vijenzi katika mchakato wa bajeti, ukijumuisha uchambuzi wa matumizi ya sekta muhimu unaofuatiwa na mada na mjadala juu ya mada iliyowasilishwa katika mkutano wa robo ya nne.

Download file .pdf


Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors