Utawalana Usimamizi wa Fedha za Afya

HEALTH CARE GOVERNANCE AND FINANCING (HGF)

Idara ya Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya inafanya kazi kufikia malengo makuu matatu; kuongeza ufanisi wa bajeti, uwazi na uwajibikaji katika Serikali kuu pamoja na Serikali za mitaa/vijiji. Katika kufanikisha malengo hayo, tunafanya kazi kwa karibu na wadau wakuu ambao ni Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ili kuchangia kuleta mabadiliko na kufikia malengo yaliyowekwa.

 Tunaamini kwamba uwazi katika bajeti utakuza ushiriki wa wananchi kwenye mchakato mzima wa uandaaji wa bajeti na hivyo kuweka umiliki wa mchakato huo mikononi mwa wananchi. Kukuza ufanisi katika mgawanyo na matumizi ya rasilimali ndani ya sekta ya afya pamoja na usimamizi mzuri, kutaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wote.

Leave a Reply

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors