Historia Yetu

 

UnknownSikika ni shirika lisilo la kiserika lilililosajiliwa nchini Tanzania kwa lengo la kufanya ushawishi na utetezi juu ya utawala bora katika sekta ya afya. Shirika lilianzishwa mwaka 1999 likijulikana kama Youth Action Volunteers(YAV), na baadaye lilikua na kubadilika kutoka katika utetezi wa  afya ya uzazi kwa vijana na kujikita kwenye maeneo makuu ya msingi katika  sekta ya afya ambayo ni: Utawala na Usimamizi wa Fedha za Afya, Rasilimali Watu katika AfyaMadawa na Vifaa tiba pamoja na UKIMWI na Virusi vya UKIMWI.

Kwa sasa, tumeimarisha shughuli zetu katika maeneo ya vijijini ambayo ni Kondoa na Mpwapwa (Dodoma), Kiteto na Simanjiro (Manyara), Iramba na SingidaVijijini (Singida) ili kukukuza na kuimarisha  juhudi zilizokuwa zinatekelezwa awali mijini na kwenye miji midogo ikijumuisha  wilaya za Dar es Salaam na Kibaha.

2013-10-10 09.20.15

Tumeendelea kufanya utafiti mbalimbali wa kisayansi na kutumia matokeo na shuhuda za tafiti hizo kufanya utetezi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya. Tunaendeleza utamaduni wetu wa kufanyakazi kwa kujitolea  na tunao wanajamii 70 wanaojitolea.  Vilevile tunatambua wananchi wote kama watumia huduma za afya. Hivyo basi, tunawezesha wanajamii wenyewe kushiriki  kikamilifu  katika Kusimamia Uwajibikaji na Kutathmini utoaji wa huduma za afya katika ngazi zote (SAM)

Sikika inatumia mbinu ya kupima matokeo ya kazi zake (Outcome Mapping) ili kutathmini mchango wa shughuli  hizo katika mabadiliko ya sekta ya afya nchini. Nguvu kubwa ya shughuli zetu za utetezi inatokana na  ubora wa utafiti tunaofanya pamoja na ushirikiano wa karibu na wadau na asasi zingine za kiraia.

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors