VVU/UKIMWI

HIV & AIDS

Idara ya VVU/UKIMWI inalenga kuhimiza uwajibikaji katika usimamizi wa matumizi ya rasilimali za UKIMWI ili kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU).

Ili kufikia malengo yake, idara hutumia mbinu mbalimbali zikiwemo uchambuzi wa mipango, bajeti na ripoti za utekelezaji za UKIMWI za serikali kuu na serikali za mitaa/vijiji ili kuhimiza matumizi sahihi ya rasilimali za UKIMWI. Lengo kuu la shughuli hii ni kuleta ufanisi katika mipango, mgawanyo wa bajeti na utekelezaji wa shughuli za UKIMWI kulingana na sera na miongozo mbalimbali. Kazi nyingine za idara ni kuhamasisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba zikiwemo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na vipimo kama CD4; kuhamasisha ufanyaji kazi wa kamati za kudhibiti UKIMWI kulingana na miongozo pamoja na kuwawezesha wananchi kudai haki zao.

Leave a Reply

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors