


Karibu sana!Sikika ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa nchini Tanzania mwaka 2000. maono ya sikika ni huduma bora za afya kwa kila mtanzania.
Sikika huwawezesha wananchi kushirikiana vema na watoa huduma za afya kwa kupitia uhamasishaji wa ushiriki wa jamii, uwazi, na uwajibikaji katika mifumo ya utoaji huduma za afya katika ngazi ya wilaya. Sikika pia hufanya kazi pamoja na bunge na wizara kuu zinazo husika kuboresha mipango ya taifa ya afaya pamoja na bajeti. Kwa sasa sikika hupatika Dar es salaam na Kibaha miji yote hii ikiwa katika ukanda wa pwani ya Tanzania Majibu ya maswali kama Serikali ina mpango gani wa kudhibiti maabukizi ya vvu / ukimwi, bajeti ya secta ya afya ikoje, wananchi wana mtazamo gani juu ya huduma za afya nchini Tanzania na je wanachi wanajua haki zao? Yanapatikana katika tovuti yetu pamoja na machapisho. halikadhalika jarida letu litakuwa linakupa taarifa juu ya kazi zetu, maendeleo pamoja na changamoto. |
MAENEO YA PROGRAMU
Usimamizi wa Afya na Fedha
Rasilimali Watu Katika Afya
Madawa na Usanbazaji
VVU na UKIMWI
|