Dawa na Vifaa tiba

MEDICINES AND MEDICAL SUPPLIES (M&S)

Idara hii ina lengo kuu la kuboresha uwepo na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba muhimu vyenye ubora katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya nchini. Lengo hili kuu limegawanyika katika malengo madogo matatu ya kiutendaji ambayo ni; kuboresha usawa na mipango ya bajeti za dawa na vifaa tiba, kuboresha ufanisi, uwazi na uwajibikaji katika ununuzi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kukuza ari ya wananchi katika kufuatilia uwepo na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma za afya vya umma hapa nchini.

Ili kuhakikisha kwamba malengo haya yanafikiwa, idara hii hufanya tafiti mbalimbali ili kupata picha halisi ya uwepo na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vyenye ubora katika vituo vya huduma za afya vya umma. Madhumuni ni kufanya utetezi kulingana na ushahidi kutoka katika tafiti zetu ili kuboresha ufanisi wa mamlaka zenye dhamana ya kuhakikisha wananchi wanapata dawa zenye viwango vya ubora, wakati wote. Mamlaka hizo ni pamoja na Bohari Kuu ya Dawa ya taifa (MSD), Kitengo cha dawa (PSS) na Mamlaka ya Dawa na Chakula Tanzania (TFDA), ambazo zote zipo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Leave a Reply

Choose your Style
Layout Style
Predefined Colors * You can use Unlimited Colors